Pages

Photography courses Announcement

Photography courses Announcement
Flame Tree Media Trust and Time School of Journalism announces Photography courses to begin soon at Talent Media Learning Centre at Ilala in Dar es Salaam, download this advert for more details.

Monday, November 1, 2010

kigoma single images


Mkoa wa Kigoma unakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa ni usafiri.

Train ndio kimbilio na msaada mkubwa kwa walio wengi, toka (1918 tangu reli hiyo ilipoanzishwa) enzi na enzi kutokana na unafuu wake.



Pamoja na kuwa ni tegemeo, usafiri huu unakabiliwa na changamoto za hapa na pale ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma bora za usafiri,uchakavu wa mabehewa pamoja na njia ya reli ambayo ni ya muda mrefu.


Jumanne Gange anaangalia changamoto hizi.

Kigoma single images



Katika miaka ya hivi karibuni nchi yetu imekumbwa na wimbi la mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino), ambayo chanzo chake kikubwa ni imani potofu za kishirikina kwa baadhi ya wanajamii, wenye kupenda utajiri wa haraka.




Hali hiyo imesababisha baadhi ya Albino nchini kulazimika kuishi katika vituo mbali mbali, mbali na jamii yao kwa kuhofia usalama wao.


Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa minajiri ya kupata viungo vyao kwa imani za kishirikina yalileta sifa mbaya sana kwa taifa letu, Boniface Mpagape alimulika kambi ya Kabanga wilayani Kasulu

Kigoma single images


Katika kipindi cha miaka kumi na sita tangu mwaka 1993 hadi 2010, kumekuwa kukiripotiwa taarifa mbalimbali za ujambazi na mauaji ya wananchi yanayofanywa na watu wanaotajwa kuwa majambazi sugu wanaotumia silaha za moto kufanya uporaji katika barabara mbalimbali na maeneo ya makazi na biashara hapa nchini.



Katika kipindi cha mwaka 2006 na 2007 jumla ya matukio ya mauaji 3583 sawa na asilimia 37.2 yaliripotiwa kwa jeshi la polisi na mengi kati ya hayo yanatajwa kusababishwa na watu kuwania mali, ubakaji, mauaji ya kishirikina, ujambazi wa utekaji wa magari na uvunjaji pamoja na wivu wa kimapenzi.



Katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wastani wa matukio 10 hadi 20 hutokea kila mwaka na kusababisha vifo vya watu na upotevu mkubwa wa mali unaofanywa na majambazi ambao huteka mgari na kuwashambulia abiria kwa risasi kwa lengo la kupora mali.




Prosper Kwigize aliangalia kwa undani tatizo hilo ikiwa ni pamoja na familia zilizokubwa na kadhia hii huko Kibondo, Kigoma.

Popular Posts

Total Pageviews