Katika miaka ya hivi karibuni nchi yetu imekumbwa na wimbi la mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino), ambayo chanzo chake kikubwa ni imani potofu za kishirikina kwa baadhi ya wanajamii, wenye kupenda utajiri wa haraka.
Hali hiyo imesababisha baadhi ya Albino nchini kulazimika kuishi katika vituo mbali mbali, mbali na jamii yao kwa kuhofia usalama wao.
Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa minajiri ya kupata viungo vyao kwa imani za kishirikina yalileta sifa mbaya sana kwa taifa letu, Boniface Mpagape alimulika kambi ya Kabanga wilayani Kasulu
No comments:
Post a Comment