Pages

Photography courses Announcement

Photography courses Announcement
Flame Tree Media Trust and Time School of Journalism announces Photography courses to begin soon at Talent Media Learning Centre at Ilala in Dar es Salaam, download this advert for more details.

Wednesday, September 29, 2010

Changamoto ya Mto Lukuledi- the full story

Na Christopher Lilai/ftmt/TMF









Ukosefu wa daraja kwenye mto Lukuledi unaounganisha Makao Makuu ya Kata ya Nyengedi na Kijiji cha Mtumbya wilayani Lindi vijijini, kunawafanya wananchi wa vijiji hivyo na wale wa kitongoji cha Mtandi kuwa na wakati kwa kipindi chote cha mwaka hasa wakati wa masika ambapo mto huo ujaa kiasi cha watu kuwa hatarini kupoteza maisha.






Wakazi hao wapatao 1,342 ulazimika kutumia usafiri wa mtumbwi na kamba kuvuka mto huo ambao una mamba wengi ili kwenda upande wa pili wa mto ambako ni makazi kwa wale wa kijiji cha Mtumbya na wa Kitongoji cha Mtandi ambacho ni sehemu ya kijiji cha Nyengendi na wale mashamba ya wanakijiji wengi wa Nyegedi.






Kwa mujibu wa wakazi wa vijiji hivyo kila mwaka watu kati ya watatu hadi watano upoteza maisha baada ya kusombwa na maji ya mto huo na wengi kunusurikana mamba.





Mmiliki wa mtumbwi ambao unatumika hivi sasa kuwavushia watu Bw. Kawanga Abuswamadi Kawanga ameleeza kuwa kila siku mtumbwi wake uvusha watu wapatao sitini ambapo uchangia kiasi cha shilingi mia moja kwa kila mtu na wale ambao ufanya shughuli za kilimo ulazimika kutoa debe moja la mazao ya nafaka ya mahindi,mtama au mpunga.




Bw Kawanga ambae ni mmoja kati ya waliowahi kushambuliwa nakujeruhiwa na mamba kwenye mto huo ameleza kuwa serikali kupitia Diwani wa kata hiyo ilipeleka mtumbwi mmoja ili kusaidia wanachi kuwavusha lakini hata hivyo mtumbwi huo ulisombwa na maji ambayo upita kwa kasi kubwa.









.Naye Afisa mtendaji wa kata ya Nyengedi,Bw,Exvery Ngomo amekiri kuwepo tatizo hilo ambalo licha ya kuathiri utendaji wake wa kazi na shunghuli za kilimo kwa wananchi wanaolima upande wa pili wa mto pia, amesema inahatarisha maisha ya wanafunzi wa kitongoji cha Mtandi ambao wanasoma shule ya msingi ya Nyengedi.





Habari hii ilitoka katika Gazeti la Mwananchi Tarehe 28/09/2010 ISSN 0856-7573 Na 03750.

No comments:

Popular Posts

Total Pageviews